Unknown Unknown Author
Title: Mo Ibrahim hatihati kutocheza dhidi ya Azam, Cheche naye asema dawa ya Simba IPO tayari
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Iddi Cheche amesema dawa ya Simba katika mechi ya fainali ya Kombe la Mapinduzi iko tayari, bado kunyweshwa tu Simba  huenda wakamkos...
Iddi Cheche amesema dawa ya Simba katika mechi ya fainali ya Kombe la Mapinduzi iko tayari, bado kunyweshwa tu
Simba huenda wakamkosa kiungo wa mshambuliaji Mohamed Ibrahim katika mechi ya fainali Kombe la Mapinduzi dhidi ya Azam FC leo.
Simba itashuka dimbani Amaan kuivaa Azam FC katika mechi ya Kombe la Mapinduzi. Azam ikiwa na rekodi ya kutofungwa hata goli moja katika michuano hiyo msimu huu.
Kocha Msaidizi wa Simba, Jackson Mayanja amesema bado hali ya Mo Ibrahim haijaimalika kwa asilimia mia.
“Kila kitu kinakwenda vizuri na maandalizi ni mazuri. Lakini Ibrahim, hali yake bado si asilimia mia. Hivyo ni suala la kuendelea kuangalia,” alisema.
Mo Ibrahim alilazimika kutoka nje na nafasi yake kuchukuliwa na Laudit Mavugo katika mechi ya nusu fainali dhidi Yanga. Simba ilishinda mechi hiyo kwa mikwaju ya penalti 4-2.
Mayanja alisema Simba inatambua mechi hiyo ni ngumu na itapambana vilivyo kuhakikisha inafanikiwa kubeba ubingwa.
Aidha kwa upande wa wapinzani wao, Kocha wa muda wa Azam FC Iddi Cheche amesema dawa ya Simba katika mechi ya fainali ya Kombe la Mapinduzi iko tayari, bado kunyweshwa tu.
Simba itashuka dimbani Amaan kuivaa Azam FC katika mechi ya Kombe la Mapinduzi. Cheche amesema maandalizi yanakwenda vizuri na Simba, haiwezi kumpa hofu.
"Imebaki kuwanywesha tu dawa yao, nimecheza na Simba wakati nikiwa mchezaji. Najua aina yao ya uchezaji, kawaida huwa haibadiliki sana.
"Naweza kusema dawa yao imekamilika na kila kitu kitakwenda vizuri," alisema.
Azam FC ambayo ilianza michuano hiyo kwa kusuasua, iliitwanga Yanga kwa mabao 4-0 katika mechi ya mwisho ya makundi na kutinga nusu fainali kwa kishindo.
Hali hiyo inaonyesha kuamsha hali ya kujiamini kwa Azam FC ambayo siku chache uongozi wake uliwatimua makocha kutoka Hispania.
 

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top