Unknown Unknown Author
Title: David Silva: Manchester City inataka ushindi dhidi ya United siyo sare
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Nyota wa Manchester City David Silva amesisitza kuwa yeye na wachezaji wenzake hawataridhishwa na chochote tofauti na ushindi watakapoika...
Nyota wa Manchester City David Silva amesisitza kuwa yeye na wachezaji wenzake hawataridhishwa na chochote tofauti na ushindi watakapoikabili Manchester United Old Trafford Jumamosi.
Mechi hiyo itakuwa ni mara ya kwanza Pep Guardiola na Jose Mourinho kukutana kama mameneja baada ya kuchukua kibarua cha kuinoa Manchester City na United.
Timu zote zinashuka dimbani zikiwa na rekodi ya ushindi kwa 100% kwani zote zimeshinda mechi zote tatu za awali katika Ligi Kuu Uingereza, lakini City wanaongoza katika msimamo wa Ligi kwa tofauti ya mabao.
"Tumeanza vizuri msimu na tunaamini utakuwa mchezo safi, lakini hatutacheza kutafuta sare," Silva alikiambia Cope.
"Tunakwenda kushinda mechi. Ni uwanja ambao mambo yalituendea vizuri miaka michache iliyopita. Tunajua kwamba ni washindani wagumu sana, lakini hatutakubali sare."
Mara ya mwisho timu hizo kukutana Old Trafford walimaliza kwa sare tasa - mara ya kwanza ndani ya miaka mitano.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top