toniking toniking Author
Title: MICHEZO Kaokoa maisha ya mchezaji mwenzake, ila FIFA wanamchunguza staili yake ya ushangiliaji
Author: toniking
Rating 5 of 5 Des:
        Beki wa klabu ya   Paris Saint Gemain   ya   Ufaransa   anayeichezea timu ya taifa ya  Ivory Coast   Serge Aurier   weekend iliyo...
       
Beki wa klabu ya Paris Saint Gemain ya Ufaransa anayeichezea timu ya taifa ya Ivory Coast Serge Aurier weekend iliyopita alipongezwa na watu wengi wa soka hususani kwa kitendo chake cha kijasiri cha kuokoa maisha cha mchezaji wa timu ya taifa yaMali Moussa Doumbia.
Serge alipongezwa na watu wengi baada ya kumsaidia Doumbia asimeze ulimi wake kufuatia kupoteza fahamu uwanjani, kitendo ambacho kingeweza kumfanya Doumbiaapoteze maisha, licha ya kitendo hicho cha kijasiri FIFA wametoa statement ya kufanya uchunguzi kwa nini Serge alishangilia staili kama ya kuchinja baada ya kufunga goli.

Beki huyo ambaye amewahi kuingia katika headlines ikiwemo kudaiwa kumtukana kwa lugha ya ishara kocha wa PSG Laurent Blanc, alifunga goli katika ushindi wa goli 3-1 kati ya Ivory Coast dhidi ya Mali na kuweka mkono kwenye shingo na kuuchezeshachezesha kama kisu wakati akishangilia goli.
sport-preview-aurier
Hapa wakati akishangilia goli lake kwa staili iliyofanya FIFA watangaze kuanza kufanya uchunguzi

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top