toniking toniking Author
Title: MICHEZO Muda atakaokaa nje ya uwanja Chidebere baada ya kuumia taya
Author: toniking
Rating 5 of 5 Des:
October 14 2016 taarifa rasmi zimetoka kuhusiana na hali ya mchezaji wa  Stand United   Abasrim Chidiebere   aliyeumia taya wakati wa mc...
October 14 2016 taarifa rasmi zimetoka kuhusiana na hali ya mchezaji wa Stand United Abasrim Chidiebere aliyeumia taya wakati wa mchezo wa Stand United dhidi ya Azam FC uliochezwa katika uwanja wa Kambarage Shinyanga na Stand United kuendeleza rekodi yake ya kutofungwa msimu huu kwa kuifunga Azam FC goli 1-0.
Wakati wa mchezo huo mchezaji wa Stand United  Abasrim Chidiebere alitolewa nje ya uwanja baada ya kugongwa katika taya na beki wa Azam FC Aggrey Morris, kupitia mtandao wa habari za michezo Tanzania wa shaffihdauda.co.tz umeripoti taarifa ya daktari kuhusu mchezaji huyo.

Nahodha wa Azam FC John Bocco alikuwa ni mmoja kati ya wachezaji wa Azam FC waliokwenda kumsalimia Chidebere
Kwa mujibu wa shaffihdauda.co.tz Chidebere ambaye kwa sasa hawezi kuongea kutokana na kufungwa nyaya maalum katika meno yake, daktari amesema atakaa nje ya uwanja kwa zaidi ya wiki mbili kwa ajili ya kuuguza jeraha hilo huku akisisitiza pia anahitaji uangalizi wa karibu kwa wakati huu.



About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top